Jumamosi 19 Aprili 2025 - 17:45
Udharura wa kuondoa mapungufu katika shughuli za Hija na Umra na kupunguza gharama za Hija

Ayatollah al-Udhma Makarim Shirazi, akiashiria udharura wa kuondoa mapungufu katika shughuli za Hija na Umra, amesisitiza juu ya kupunguzwa kwa gharama za Hija na muda wa safari ya Hija ya Tamattu' kwa mahujaji wa Kiirani, pia juu ya kuwepo kwa urahisi wa kimaanawi katika safari za Umra za Ramadhani, na kufanya matumizi ya rasilimali kwa njia bora na yenye ufanisi zaidi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Makarim Shirazi, katika kikao chake na msimamizi wa mahujaji wa kiirani, alieleza kuwa kuhudumu katika nyanja ya Hija na Ziara ni jambo lenye thamani kubwa sana, na alisifu usimamizi mzuri, uzoefu wa muda mrefu na nia njema ya mwakilishi wa kiongozi mkuu wa dini (Waliyyul-Faqih) katika jukumu hili, na akasema: Natumai kwa usimamizi wenye ufanisi na mafanikio, masuala ya Hija na ratiba za mahujaji zitafanyika katika njia inayofaa na nzuri, ili kupara radhi za wenye kuizuru nyumba ya Mwenyezi Mungu.

Mwanazuoni huyu mkubwa (Marja’ Taqlid), akiashiria ulazima wa kuondoa mapungufu katika shughuli za Hija na Umra, alisisitiza juu ya kupunguzwa kwa gharama za Hija na muda wa safari ya Hija ya Tamattu' kwa mahujaji wa Kiirani, pamoja na kuwepo kwa urahisi wa kiroho katika safari za Umra za Ramadhani, na matumizi ya rasilimali kwa njia yenye ufanisi zaidi na bora.

Mwisho wa mazungumzo yake, alisisitiza juu ya umuhimu wa dua na kutawassali kwa upande wa mahujaji na wahudumu wa Hija kwa ajili ya kutatuliwa kwa matatizo yanayo ukabili ulimwengu wa kiislamu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha